JIFUNZE KUANDAA MTINDI
UTAYARISHAJI WA MTINDI NYUMBANI :
Wafugaji wengi wamekuwa wakiuliza mbinu za kutayarisha mtindi nyumbani. Hii inatokana na ukweli kwamba wakati wanapata ziada ya maziwa wanayozalisha na soko la maziwa kupungua hufikiria namna nyingine ya kuokoa ziada hiyo isiharibike kwa kutengeneza bidhaa nyingine.
Mtindi unaotayarishwa nyumbani kwa kawaida huwa mtamu na huweza kutumika muda wowote wa mchana kama vile nyongeza nyepesi ya kifungua kinywa au kutumika kama kinywaji cha kuboresha afya zetu kwa kuchanganywa na asali au matunda na kuweza kunywewa nyakati za jioni. Vilevile itabidi ifahamike kwamba unapokunywa mtindi huu utafaidika na vijidudu rafiki vya bakteria vilivyomo katika kinywaji hiki ambao husaidia kuboresha utendaji kazi wa mfumo mzima wa usagaji chakula mwilini.
Mtindi unaotayarishwa huwa na virutubisho vingi na ni rahisi kuutayarisha hata kwa kiasi kidogo tu kuliko mtindi wa viwandani ambao huchemshwa sana kwa majiko ya umeme.
MAHITAJI
VIAMBATO
• Lita moja ya maziwa freshi
• Mtindi fresh usio na mchanganyiko wa kitu chochote vile kama matunda au ladha itakayotumika kama kianzio (starter) au waweza kutumia mtindi wa kiwandani kama kianzio cha mazaliano (culture) ya vijidudu hivi vya bakteria ambavyo ni rafi ki kwa binaadamu.
VIFAA VINAVYOHITAJIKA
• Chungu safi cha kuchemshia maziwa
• Chombo (container) ambacho utaweza kuhifadhi mtindi unaoendelea kuchachuka (fermenting) na liwekwe katika hali ya uvuguvugu ili kuwezesha vijidudu hivi kwenye mtindi viendelea kufanya kazi vizuri. Chombo hiki kifunikwe kwa mfuniko safi na itabidi izingatiwe kwamba usitumie chombo cha aluminium isipokuwa lazima kiwe cha udongo kama mtungi, chombo vya udongo (glass) au vya plastiki.
• Safisha vyombo hivi vizuri na usuuze kwa maji ya moto kabla ya kuanza kutumia.
• Na kama utaweza kupata kipima joto cha kupikia (Cooking thermometer) basi unaweza kukitumia pia.
NAMNA YA KUTAYARISHA MTINDI
1. Chemsha maziwa mpaka yafi kie nyuzijoto 850C au karibu ya kuchemka. Hakikisha unakuwa makini kuangalia maziwa yako na kuyakoroga wakati wote yanapokuwa yanachemka. Na kama utakuwa kuna kipima joto basi utaweza kutambua kama maziwa yako yamefi kiwa nyuzijoto 850C kwa maziwa kuanza kufura (froth).
2. Yaondoshe kutoka kwenye jiko na yaache yapoe mpaka kufi kia nyuzijoto 450C. Hivyo kuwa na bafu la maji ya baridi litasaidia kupooza joto hili sawasawa na haraka na kuhitaji tu kukorogwa kwa muda fulani. Kwa nyuzijoto 450C mfugaji anaweza kutambua kwa kuhisi joto la chombo husika kuwa juu kidogo la joto la kawaida la mwili. Epuka joto kuwa juu ya kiwango cha nyuzijoto 450C wakati wote kwa sababu
kiwango hicho kitaua vijidudu hivi muhimu vya bakteria.
3. Wakati unasubiri maziwa yako yapoe, uache mtindi wako wa kuanzia (starter yoghourt) kwenye joto la kawaida la chumba. Hii itaepusha
mtindi huu kuwa wa baridi sana wakati utakapouchanganya kwenye maziwa.
4. Changanya mtindi wa kuanzia kwenye mtindi wako unaoutayarisha na ukoroge vyema na kama ikiwezekana kwa kutumia chombo maalumu cha jikoni cha kuchanganyia (wire whisk) na mtindi wa kuanzia kiasi cha gramu 15 utaweza kutosha kwa lita mbili za maziwa.
5. Mimina mchanganyiko huu kwenye chombo safi ulichokitayarisha kwa ajilia kuatamizwa (incubation) funika chombo na ukiweke sehemu ya joto la wastani ili kuwezesha bakteria waliomo katika mchanganyiko huu waweze kukua (joto linalopasa kutumika likaribie nyuzijoto 420C ikiwezekana. Na kama hutaweza kuwa na jiko la oven lenye kidhibiti joto unaweza kuweka kwenye sufuria kubwa la kupikia liliojazwa maji ya vuguvugu.
Iwapo joto la maji litakuwa chini ya joto la kawaida la mwili, basi itapasa uweke sufuria hii yenye maji karibu na moto. Lakini itakulazimukuhakikisha kwamba maji yako hayapati joto kupita kiwango kilichoshauriwa hapo juu.
6. Iwapo utakosa muda wa kuweza kusimamia mtindi wako kwa masaa basi itapasa lifunike pande zote na upande wa juu wa sufuria hili kwa kutumia blanketi zito na lenye joto. Uache hivyo bila kutingishwa kwa masaa kadhaa. kwa wastani masaa 4 mpaka 5 na hakikisha hauchi muda mrefu zaidi ya huo la sivyo mtindi wako utakuwa mchungu na hautapenda kuunywa. Na uhakikishe mtindi wako umekuwa mzito.
7. Mtindi wako unaweza kutumika au kuhifadhiwa ndani ya jokofu kwa muda wa juma moja na kama hutaweza kuhifadhi kwenye joto la kiwango cha chini (jokofu) basi itakulazimu uutumia kwa siku moja tu.
8. Ongezea matunda na sukari kulingana upatikanaji wa vitu hivi na ladha ya mtindi ambayo ungetaka kuipata.
MTINDI WA KUANZIA (STARTER):
Ni vema basi tukaongea kidogo kuhusu mtindi wa kuanzia: Unaweza kutumia mtindi huu uliokwisha tayarisha kama kianzio (starter) kwa mkupuo (Batch) wa uzalishaji unaofuata. Lazima inapasa kufahamu kwamba haitawezekana kutumia mtindi kuzalisha mikupuo mingi ya uzalishaji inayofuata kwa vile kadiri inavyotumika idadi ya bakteria waliomo na ambao ndiyo wanaofanya kazi ya kuyachachua (ferment) maziwa huwa inakuwa imepungua (deteriorate) sana kiasi cha kushindwa kushindwa kufanya vema shughuli hiyo.
Hivyo inapendekezwa kutumia mtindi mpya kutoka madukani au kununua kianzio maalum cha kukuzia bakteria kama utaamua kuwa unatengeneza mtindi mara kwa mara na kiasi kikubwa kwa ajili ya kufanya biashara.
No comments: